MTU
ALIYEKUWA TAJIRI NA HAKUBAHATIKA KUPATA MTOTO WA KUMFAA
Imesimuliwa na Ngwali Mashaka
Hapo zamani za kale
alikuwepo bwana mmoja aliyekuwa akiitwa Hassan Saira. Bwana huyo alikuwa ni tajiri sana kwa wakati
wake. Vile vile alikuwapo mtu mmoja katika kijiji hicho ambae ni masikini sana
bwana huyo alikuwa akiitwa Bwana Vuai Pandu. Bwana Hassan ni mtu mmoja wapo
aliyepewa uwezo mzuri na Mwenyezi Mungu.
Bwana huyo alioa na akapata mtoto mmoja wa
kiume aliyeitwa Maulid. Mtoto wake huyo alikuwa ni mgonjwa, lakini moyo wake
ulipenda amuozeshe na huenda ikawa bahati nzuri akapoa na kupata mtoto ambaye
aliweza kumfaa babu yake. Bwana Hassan alikwenda kwa jirani yake Bwana Vuai
Pandu ambaye alikuwa na watoto wengi wake na waume. Bwana Hassan alikwenda kuposa
katika nchi moja wapo ya kifalme na kumwambia mzee Vuai kuwa mtoto wangu
nimemposea lakini ni mgonjwa haifai kuonekana. Lakini nimekuja kwako unipe
mtoto wako mmoja aitwae Yunus. Bwana Vuai alisema na kumwambia Bwana Hassan
mimi mtoto wangu ni masikini jee atawezaji kufika kutoka nchi hizo za kifalme
na akaonekane kuwa ni mtu? Bwana Hassan alijibu kuwa ataonekana kuwa ni mtu,
usijali.
Bwana Vuai alimuelezea mkewe Bibi Khadija
kadhia hiyo. Bi. Khadija alimwambia mumewe jee haitakuwa taabu baada ya
kwishakuoana, kwa sababu kila mmoja atakuwa anampenda mwenziwe? Mzee Vuai alisema si tatizo nitamnasihi sana
baada ya kurudi hapa tu kuwa amwache. Hapo alimwambia asili ya kukwambia hayo
sisi hapa ni masikini tusipokubali anaweza hata kutufukuza, tutafanya
nini? Kwa hiyo ni bora tukubali. Baada ya maneno hayo Bi Khadija aliridhika na
Bwana Vuai alipeleka jawabu kwa Bwana Hassan Saira kuwa ameridhika kumpa mtoto
wake. Na hapo ilifanywa safari, akasafi ri kwa meli, huku mtoto wa Bwana Vuai
akapambwa na kuonekana ni mtoto wa mfalme. Pia askari walichukuliwa wakenda
kwenye harusi. Mizinga ilisikika siku ile ya kupokewa bwana harusi na
kukaribishwa wapite ndani ya kasri ya Mfalme. Gari nyingi za watu zilikuja
katika sherehe hiyo na mtoto wa mfalme akachukuliwa na kufanyiwa kama ilivyo
ada ya harusi na wafalme wote waliohudhuria walifurahi sana kwa kupata mchumba
mzuri wa kifalme.
Baada ya hapo
ilifanyika safari ya kurudi nyumbani ambapo alikabidhiwa watumishi mbali mbali,
wa kike na wanaume. Mizinga ya harusi ya kurudi ilisikika na watu wote walikuja
kumpokea harusi. Shangwe na vigelegele vilizagaa mtaani kwa Bwana Hassan Saira.
Na walipofi ka maharusi nyumbani kwao watu walikaa na kushereheka usiku wa
kucha. Ilipofi ka siku ya pili Bwana
Vuai alikwenda kuomba kuonana na mwanawe Yunus. Yunus hakupinga amri ya mzee
wake na hapo Yunus akamuaga mkewe kuwa anakwenda kuangalia bustani zake na
alitoka nje kwa muda mchache na hatimayae mtoto wa mfalme akaletewa mume
mwengine na kuambiwa huyu ndie mumeo. Bi harusi alisema huyu siye mume wangu
niletewe mume wangu na hapo alilia kwa muda mrefu na kilio kilizagaa katika
nyumba mpaka watu wote wakatetemeka.
Aliitwa Bwana Hassan na
kuelezwa kuwa Bi harusi hataki lolote na anataka kurudi kwao au aletewe mume
wake kwani aliyeletewa siye mumewe halisi. Bwana Hassan alipofi ka mabibi wa
nyumbani walimwambia utuletee mume wetu kwa haraka. Si hivyo tunakwenda
zetu. Ikabidi Bwana Hassan kusema kuwa
huyu ndiye mume wako lakini bibi harusi akasema aitwe baba yake mzazi. Bwana Hassan alipeleka barua ya ugonjwa ili
kumrudisha kwao kwa sababu tu hataki kukaa na mume aliyekuwa siye aliyeozeshwa.
Mfalme alipopata barua
na kufi ka kule nyumbani aliletewa mwanawe. Baada ya kuzungumza na watu wa
nyumbani alihisi kuwa hana sifa ya ugonjwa. Hivyo bwana mfalme aliandika barua
ya kumshitaki Bwana Hassan kwa kitendo alichokifanya ambacho si cha ukweli.
Bwana Hassan alishitakiwa na kutakiwa kulipa fi dia kwa kitendo alichokifanya
cha kuozeshwa mtu mgonjwa .
Bwana Hassan alikubali
na kulipa fedha pamoja na masharti yote aliyopewa. Baada ya hapo mtoto wa
mfalme alimwambia mzee wake kuwa alifanya hadaa tu kumletea mtu mzima na baadae kupewa mbovu, kwa hivyo mimi ninamtaka yule
niliyeozeshwa mwanzo. Nina hakika bado kijana
yule hajafa katika nchi ile, hivyo nikaozeshwe yule yule na niletewe mwenyewe.
Kwa kweli mfalme
alisononeka sana kwa kitendo hicho kwa sababu mtoto wake alikuwa hali wala halali.
Mfalme alitoa askari na kwenda kwa Bwana Hassan Saira na kumtaka apewe yule kijana
aliyekuja kumuozesha mwanawe na wampeleke kule aliko mwana wa mfalme. Hapo
Bwana Hassan alikwenda kwa Bwana Vuai na kumwambia kuwa mfalme amekuja na
anamtaka yule kijana wako tumpelekee.
Lakini Bwana Vuai
alimwambia Bwana Hassan kuwa mwambie mfalme aje mwenyewe na asitume askari.
Baada ya hayo askari walipeleka ujumbe na mfalme akaja kutokana na shida ya
mwanawe. Mfalme baada ya kufi ka kwa Bwana Hassan, akapelekwa kwa Bwana Vuai
Pandu. Bwana Vuai alitakiwa kumwita
mtoto wake ili waende pamoja. Walipofi
ka alisema; „nasikia umetuma ujumbe kuwa nije mwenyewe nisitumize mtu yeyote,
kwa hivyo tayari nimekwishafi ka.” Hapo Bwana Vuai alisema huyu ndie mtoto
wangu alichukuliwa kwa hadaa ili kuozeshwa mtoto wako. „Jee wewe ukiangalia
anastahiki kuchukuliwa kuja huko?”
„Unakuja kuchukua
mtoto wangu, kutokana na umasikini tulio nao hebu twende ukaangalie nyumba yetu
ilivyo tunavyoishi,” alisema. Mfalme alikubali hayo yote na baada ya kufi ka
aliona nyumba yao na alimwambia warudi tena kwa Bwana Hassan. Na baada ya kufi
ka aliamrisha aletewe yule motto aliyekuwa mgonjwa, kwa kweli mfalme
alisikitika sana baada ya kuona hali yake. Baadae mfalme alizungumza na Bwana
Vuai juu ya shida iliyompata kutokana na mtoto wake, hivyo ninakiri umasikini
wako na kwamba nitakujengea nyumba yako na nitakusaidia kama ipasavyo lakini
mtoto wako amuoe mtoto wangu, kwa sababu ninaridhika vya kutosha. Na hapo Bwana
Vuai alikubaliana na mfalme na wakaandikiana mkataba kuhusu hayo
waliyoyazungumza.
Ilipofi ka siku ya
sita mfalme alifi ka na zana zote, na kuanza shughuli za ujenzi. Na baada ya
siku kidogo nyumba ilimalizika na kwenda kufunga ndoa. Hapo tena baada ya ndoa
mtoto wa mfalme alipoa matatizo yake na hatimae mtoto wa Bwana Vuai alipewa
mali nyingi sana na mfalme na unyonge pamoja na umasikini waliokuwa nao awali
ukaondoka na akawa wakati wowote anaruhusiwa kwenda kuwaona wakwe zake.