WIZI MBAYA
Imesimuliwa na Zubeda
Abdalla Omar.
Hapo zamani za kale
alikuwepo bwana mmoja, aliekuwa na wake watatu mmoja alikuwa mwizi. Yule
bwana alikuwa anafuga
mbuzi, siku moja kati ya wale wake zake mmoja aliiba mbuzi na kumchinja na kumpika bila ya yeye
kujua. Aliporudi safari yake aliuliza nani alimchinja mbuzi? Wote walikataa.
Yule bwana akasema basi
mimi nitafanya dawa. Wakajibu sawa, yule bwana akafanya mambo yake kisha akawapeleka mtoni.
Walipofika aliwambia mmoja mmoja
aanze kuingia mtoni na huku akiimba.
Aliingia wa kwanza
huku akiimba nyimbo:
Kachiriri, kachiriri kachiriri kachiriri
kachiriri.
Mani nenga Kachiri
Depala dipolo kachiri
Dipolo dabambo kachiriri
Kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri
kachiriri.
Alipomaliza kuimba
akaibuka, kwani yeye hakuwa mwizi. Akafuata wa pili huku akiimba:
Kachiriri, kachiriri kachiriri kachiriri
kachiriri.
Mani nenga Kachiri
Depala dipolo kachiri
Dipolo dabambo kachiriri
Kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri
kachiriri.
Yeye pia akaibuka na
kukaa pembeni. Akafuata yule wa tatu
akaingia huku akiimba:
Kachiriri, kachiriri kachiriri kachiriri
kachiriri.
Mani nenga Kachiri
Depala dipolo kachiri
Dipolo dabambo kachiriri
Kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri
kachiriri.
Lakini yeye alizama.
Kuona vile yule bwana
akajua kwamba yule mke wa tatu ndie mwizi. Hapo akafanya dawa zake na yule bibi akaibuka, alimuomba radhi mumewe na kuahidi
kuwa hatorudia tena kosa lake. Na yule
bwana alikubali na wakaendelea kuishi kwa raha
mustarehe.
No comments:
Post a Comment