BIASHARA YA KIFO
sehemu ya 03
Alijulikana kwa jina
la Pius Massawe, Mchaga kutoka mkoani Kilimanjaro, alikuwa kijana mwenye sura
nzuri kiasi kwamba wanawake wengi wakatokea kumpenda kutokana na uzuri wa sura
aliokuwa nao.
Wasichana wengi
kutoka katika Shule ya Sekondari ya Majengo mkoani humo walivutiwa na Pius
lakini kijana huyo hakutaka kabisa kujihusisha na mambo ya mapenzi kabisa.
Wasichana hao hawakutaka kuvumilia, waliamua kumfuata na kumwambia ukweli
kwamba walikuwa wakimpenda lakini Pius hakutaka kukubaliana nao, aliwakataa
kitu kilichowafanya watu wengi kumshangaa.
Uvumi ukaanza
kusikika kwamba Pius alikuwa akishiriki mapenzi ya jinsia moja, uvumi huo
ulivuma kwa kasi lakini yeye mwenyewe hakutaka kulizungumzia suala hilo, alijua
kwamba kulikuwa na maneno mengi yangesemwa, kwake, hizo zote alizichukulia kama
changamoto.
Mbali na uzuri wa
sura aliokuwa nao, Pius alikuwa na uwezo mkubwa darasani, katika kila mtihani,
alikuwa akiongoza kitu kilichowachanganya watu wengi kabla ya kugundua kwamba
mtu huyo alikuwa na akili za kuzaliwa, yaani kile alichokuwa akifundishwa leo,
hakuweza kukisahau hata kama ni miaka mingapi ingepita.
Wanawafunzi wengi
walikimbilia kwake kufundishwa, Pius hakuwa na maringo, alimfundisha kila mtu
japokuwa wanawake wengi walitumia njia hiyo kumtongoza lakini bado msimamo wake
ulibaki kuwa uleule kwamba asingeweza kutembea na msichana yeyote yule shuleni
hapo.
“Kwani tatizo nini
Pius?” aliuliza msichana Thedosia, japokuwa alisifika kwa uzuri shuleni hapo
kwa upande wa wanawake, lakini kwa Pius alionekana si chochote.
“Ninataka kuwa
padri.”
“Kweli?”
“Ndiyo!”
“Kwa hiyo hautooa?”
“Hakuna tatizo.
Siwezi kufanya mapenzi na msichana yeyote,” alisema Pius huku akimwangalia
msichana huyo usoni.
Huo ndiyo ulikuwa
msimamo wake, hakutaka kufanya mapenzi na msichana yeyote yule. Pius alikuwa
kijana wa tofauti na wengine, alihusudu sana ibada, kila siku alipokuwa
akihitajika kwenda kanisani, alikwenda, alipofika huko, alikaa katika kiti cha
mbele kabisa na kuanza kusali.
Kila alipokuwa,
rozali ilikuwa mkononi mwake, na kama haikuwa mkononi, aliichukua na kuivaa
shingoni. Alikuwa hivyo, nyumbani napo kulikuwa kama shuleni. Uzuri wa sura
yake ulizidi kuwatetemesha wanawake wengi, wengine walijipendeza waziwazi
lakini hakuwa na habari nao, alichokuwa akikihitaji ni kuwa padri tu.
Alipomaliza kidato
cha nne na kujiunga na cha tano katika Shule ya Sekondari ya Tambaza iliyokuwa
jijini Dar es Salaam. Kila alipofika, Pius alikuwa gumzo, japokuwa alipokuwa
mkoani Kilimanjaro aliambiwa kwamba atakapofika Dar es Salaam basi msimamo wake
ungeweza kulegea lakini huko akawa vilevile kiasi kwamba watu wakampa jina la
padri kitu kilichomfurahisha mno.
Alipomaliza kidato
cha sita kwa masomo ya kawaida, akafaulu lakini akajiunga na chuo cha upadri
kilichokuwa Morogoro na kisha kuanza masomo rasmi. Haikuwa kazi ngumu,
alizingatia masomo yake, kila siku asubuhi alikuwa akiamka na wenzake na kwenda
kanisani kusali, walipomaliza na ndipo walipoendelea na mambo mengine.
Alisoma huko kwa muda
wa miaka mitatu na ndipo walipoandaliwa kwenda kumalizia masomo ya mwisho
katika Jiji la Venice nchini Italia. Ilikuwa furaha kwake kwani alibakiza hatua
chache kabla ya kufika pale alipotaka kufika.
Kutoka Venice mpaka
Vatican haikuwa mbali sana, mara kwa mara alikuwa akielekea huko na kukutana na
viongozi wa dini ya Kiroma na kuzungumza nao mawilimatatu kitu kilichomfanya
kujisikia vizuri na kuahidi kushinda kile kilichobakia mbele yake.
Huko ndipo alipopewa
jina la Benedicto badala la lile la Pius alilokuwa akilitumia kabla. Baada ya
kukaa huko Venice kwa miaka miwili ndipo aliporudi nchini Tanzania na kupewa
kanisa huku akijulikana kwa jina la Padri Benedicto.
Kanisa likajaza
wanawake wengi kuliko wanaume, tetesi zilizokuwa zikisikika kwamba kanisa hilo
lilikuwa na padri aliyekuwa na sura nzuri iliwachanganya wanawake wengi na
hivyo kutaka kwenda huko kushuhudia kwa macho yao.
Walipomuona,
waliamini kwamba duniani kulikuwa na wanaume wenye sura nzuri mno, kila
walipomwangalia padri wao, walimtamani mno.
“Jamani hii sheria ya
mapadri kuoa si ipitishwe tu, nahisi kama bahati inaweza kuniangukia,”
alisikika akisema msichana mmoja.
“Bahati ya nini?”
“Kuolewa na padri
Benedicto, ninampenda sana jamani!”
“Wewe Upendo,
humuogopi Mungu!”
“Namuogopa, lakini
kwa nini ameamua kutupa jaribu kubwa namna hii?”
Padri Benedicto
alikuwa akiishi peke yake nyumbani kwake, wafanyakzi wengi wa ndani aliokuwa
akiwahitaji walikuwa wa kiume tu ambao wengi alikorofishana nao na mwisho wa
siku kuwafukuza kihekima.
Baada ya kufukuza
wafanyakazi watano, akaamua kuishi peke yake, hakutaka tena kuwa na mfanyakazi
yeyote nyumbani kwake kwani aliona kama angeweza kufanya kazi peke yake pasipo
mfanyakazi yeyote yule.
“Ila kuna msichana
ana matatizo sana, naomba aje akusaidie padri,” alisema mama John, mwanamke
aliyekuwa ameonana na Irakoze.
“Nimsaidie vipi?”
“Aje kufanya kazi
hapa!”
“Msichana?”
“Ndiyo!”
“Hapana! Haiwezekani
hata kidogo.”
Japokuwa padri
Benedicto alikataa lakini mama John hakuacha kumbembeleza akubaliane naye kwani
mtu kama yeye alihitaji mfanyakazi wa kike kwa ajili ya kufanya usafi wa nyumba
muda wote kitu ambacho kwa kiasi fulani kikaanza kumuingia padri huyo.
Mbali na kumwambia
hivyo, pia alimsimulia historia ya kusikitisha ya msichana Irakoze kiasi kwamba
padri akaingiwa na huruma na kuona kwamba kumsaidia msichana huyo ilikuwa kama
baraka kwa Mungu kwa kuwa ameamua kumtoa mtu fulani kutoka sehemu moja ya chini
na kumuweka sehemu ya juu.
Wakakubaliana na
hivyo mama John kuelekea nyumbani ambapo akamchukua Irakoze na kuelekea naye
nyumbani hapo.
“Ni mzuri mno,
sijawahi kuona mwanaume mzuri kama huyu,” alijisemea Irakoze katika kipindi
alichomuona padri Benedicto kwa mara ya kwanza.
Hiyo ndiyo ikawa siku
ya kwanza kukutana kwa watu hao, Irakoze akaanza kazi ndani ya nyumba hiyo.
Alikuwa msichana mwenye heshima kubwa, kila siku alikuwa mtu wa kuvaa mavazi
marefu ambayo aliamini kwamba yasingemtia majaribu padri huyo.
Waliheshimiana mno,
kila siku asubuhi walikutana sebuleni, walishikana mikono na kuanza kusali
kisha kuendelea na ratiba nyingine. Katika kipindi chote hicho, Irakoze alikuwa
kwenye mapenzi ya dhati kwa padri huyo, alitamani kumwambia ukweli kwamba
alimpenda lakini aliogopa kufanya hivyo, akabaki akiugulia moyoni mwake tu.
Siku zikaendelea
kukatika, heshima ilikuwa kubwa ndani ya nyumba, Irakoze aliendelea kufanya
kazi ndani ya nyumba hiyo huku kila siku akijitoa kitendo kilichomfurahisha
padri Benedicto kiasi kwamba alijiona kuchelewa mpaka kuchukua uamuzi wa
kumuajiri mfanyakazi wa kike.
“Nakuja, niandalie
chakula,” alisema padri Benedicto.
Siku hiyo hakuwepo
nyumbani, alikuwa kanisani akiendelea na huduma, mawingu mazito yalitanda
angani kuonyesha kwamba muda wowote ule mvua ingeweza kunyesha. Mara baada ya kumaliza
kila kitu likiwa suala la kupika chakula, Irakoze akachukua khanga yake na
kuelekea bafuni kuoga.
Alipokuwa huko,
akasikia mvua kubwa ikianza kunyesha huku kiubaridi kikianza kuongezeka.
Alichokifanya Irakoze, akatoka bafuni na khanga yake kisha kutoa ndoo nje kwa
ajili ya kukinga maji ya mvua yaliyokuwa yakidondoka.
Mwili wake ukalowa,
khanga ikanata mwilini mwake, umbo lake lenye mvuto, makalio yaliojaajaa yakawa
yanaonekana vizuri kabisa. Hakuwa na wasiwasi wowote ule, alikuwa peke yake
nyumbani hapo hivyo aliendelea kufanya kazi yake.
Wakati yupo hapo
akiendelea kukinga maji, mara geti likafunguliwa na padri Benedicto kuingia.
Irakoze hakumuona padri huyo, aliendelea kukinga maji huku wakati mwingine
akijimwagia, kifua chake kikanata kwenye ile khanga, kila kitu mwilini mwake
kilionekana wazi.
Padri Benedicto
alipoona hivyo, moyo wake ukashtuka, hakupiga hatua, alibaki akimwangalia
Irakoze huku akiwa na mwamvuli wake. Alibaki akimeza mate na maeneo ya zipu
yake kuanza kusogea mbele. Alichanganyikiwa, kila alipojitahidi kuyaamisha
macho yake, yaligoma kabisa kuhama.
Mpaka Irakoze
anageuka na kumwangalia padri huyo, alikuwa hoi, kwa kujishtukia, Irakoze
akamsalimia na kisha kuelekea ndani, sehemu ya nyuma ilikuwa ikichezacheza,
padri akaona haiwezkani, japokuwa hakuwahi kulala na mwanamke yeyote maishani
mwake, uzalendo ukamshinda, pepo la ngono likamwingia, mwili wake ukaanza
kumsismka huku akihisi vijidudu fulani vikianza kumtembelea mwilini mwake, naye
akaanza kuelekea ndani huku akiwa amechanganyikiwa kimahaba, pepo la ngono
lilishamvaa, hakukubali, alitaka kuonekana kwamba hata na yeye alikuwa
mwanaume.
INAENDELEA...
No comments:
Post a Comment