Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo imetangaza orodha ya Awamu ya Nne yenye wanafunzi 1,775 wa Mwaka wa Kwanza waliofanikiwa kupata mikopo na hivyo kufanya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo hadi sasa kufikia 31,353. Katika Awamu ya Kwanza, wanafunzi 10,196 wa mwaka wa kwanza walipangiwa mikopo, Awamu ya Pili (11,481) na Awamu ya Tatu (7,901).
Orodha hiyo ya Awamu ya Nne inapatikana hapa. Aidha, orodha hii inapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz) na imeshatumwa kwa vyuo husika ili kuwawezesha wanafunzi kufanya usajili na kuendelea na masomo.
Kiasi cha shilingi 427.54 bilioni zimetengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi kwa mwaka 2017/2018 na kati ya fedha hizo shilingi 108.8 bilioni ni kwa ajili ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza. Tayari Serikali imeshatoa shilingi 147.06 bilioni kwa ajili ya robo ya kwanza ya mwaka huu wa 2017/2018.