Saturday, 5 November 2016

THE A TO Z PRINCIPLE

To Achieve Your Dreams, Remember Your A to Z


A
Avoid negative sources, people, places, things and habits.
B

Believe in yourself.
C
Consider things from every angle.
D 
Don’t give up and don ’t give in.

E

Enjoy life today— yesterday is gone, tomorrow may never come.
F

Family and friends are hidden treasures, seek them and
enjoy their riches.


Sunday, 30 October 2016

ENJOY WITH FLOWERS

ENJOY WITH FLOWERS







MUME WA AJABU

Mume wa ajabu
Imesimuliwa na Farasha Saidi Kombo

Hapo zamani za kale alikuwepo Makame wa Makame ambaye aliishi na mkewe, Mize wa Mize pamoja na watoto wao wengi. Mmoja miongoni mwa watoto wake wa kike aliolewa katika kijiji kingine cha mbali, na mtu mmoja ambaye hakujulikana mapema kama alikuwa shetani. 
Bila ya kujua mkewe alimzalia mumewe, aliyekuwa na umbo la binaadamu watoto wawili. Siku moja
mume alimuomba mkewe kwenda kumchukua mdogo wake wa kike ili aje kumsaidia kazi za nyumbani.

Mke alikubali kutokana na kuwa na kazi nyingi sana za ndani na shambani ambazo hakuweza kuzikamilisha akiwa peke yake.  Kwa hivyo mwanamke alifanya kama alivyotakiwa na kwenda kumchukua mdogo wake wa kike. Kuanzia hapo mdogo wake wa kike alibaki nyumbani na watoto na yeye kufanya kazi shambani. Siku moja mumewe alirudi nyumbani ghafla na kumwambia shemeji yake kwamba alitaka kwenda kusali.

Wakati huo shemeji yake alikuwa akitwanga mtama. Lakini yule bwana hakutoka nyumbani bali
alijificha sehemu ambapo aliweza kusikia mtama ukitwangwa. Yule bwana, ambaye alikuwa shetani hakupenda chengine zaidi ya ule mlio wa kutwanga. Yule bwana alipogundulika kuwemo ndani ya nyumba, alimwambia shemeji yake kwamba alikuwa akisikiliza mlio wa kutwanga, ambao ulikuwa mlio takatifu na hairuhusiwi mtu yeyote mwingine kujua.

Alimlazimisha kuimba nyimbo ifuatayo akiwa anatwanga: „Rudia na endelea kutwanga mtama, sina kazi, lakini ninafanya kazi na rafiki zangu.” Yule bwana alifurahia sana kitendo hicho na kumfanya kuwepo kila siku, wakati mtama ukitwangwa na nyimbo ikiimbwa. Alijificha katika chumba kingine ambacho alidiriki hata kucheza.
Siku moja shemeji yake alimgundua akiwa anacheza ngoma ya mashetani. Alishtushwa na kushindwa kuamini macho yake na kuamua kurudi nyumbani kwao na kuanza kuwasimulia watu. Siku moja alimtaka dada yake kurudi mapema nyumbani ili aweze kujionea mwenyewe mambo
yanayofanywa na mume wake.
Ilipofika jioni, yule mwanamke alimuelezea mumewe madai aliyotoa mdogo wake.
Kama kawaida yule mwanamke alipigwa na butwaa  na kuendelea kudadisi.

Siku iliyofuata yule bwana alimtaka shemeji yake kutwanga mtama huku akiwa anaimba ili aweze kucheza ngoma yake ya mashetani.
Kitendo ambacho kilisababisha mkewe aendelee kuwaeleza majirani kisa chote. Hatimaye aliwataka majirani kufika nyumbani wakati wa sala na kujificha na kujionea wenyewe kilichokuwa kikifanywa na mumewe. Kwa huzuni wale wanawake walikubali kufuata maelekezo waliyopewa.Yule bwana alipofika nyumbani wakati wa sala na kutaka kuanza kucheza ngoma yake ya kichawi, wale wanawake waliokuwa wamejificha waliibuka na kumpa maneno yake. Yule bwana ghafla alijigeuza shetani akiwa katika umbo la ndege na chura na kutoweka huku akiiacha familia yake ikiwa pweke nyumbani.