Friday 28 October 2016

WAHENGA WETU!!

Ganda la muwa la jana, chungu kaona kivuno 
Ganda la jana la muwa huwa limekauka, lakini chungu anapolipata huona ni mavuno maridhawa. Maana asiyezoea kuwa nacho, akipatapo hata kama ni kitu duni au hafifu namna gani na kidogo, hushangilia. Mathalani, kukengeuka kwa maadili kwa vijana barani Afrika na kuzamia tamaduni za kigeni.

Milima haikutani, lakini binadamu hukutana
Milima haina uwezo wa kukutana, lakini binadamu wakiwa hai huweza kukutana hata baada ya kuwa mbalimbali kwa muda mrefu. Hii ni methali inayotumika katika kutiana moyo wakati wanapoagana kwamba wakijaliwa watakutana. Pia hutumika katika kuwaonya watu kuacha tabia ya kuwatendea vibaya wengine kwani huenda wao pia wakatendewa hivyo siku za usoni. 

No comments:

Post a Comment