RUDI 03
HUSSEIN O. MOLITO
Kwa james ilikua ni
kitu kingine kabisa baada ya kuruhsiwa kuushika mkono mlaini kabisa wa Jasmini
huku tabasamu alilo liachia likimfanya James ahamie dunia nyingie. Hakumuachia
haraka hadi pale Jasmini alipotumia nguvu kidogo kuutoa mkono wake na kumfanya
James kurudisha network zake zilizopotea kwa sekunde kadhaa baada ya kushikana
tu mikono na kuangaliana usoni.
“karibu sana
Jasmini.. jisikie upo nyumbani.” Aliongea James na kumfanya Jasmini atabasamu
na kwenda kukaa kwenye moja ya masofa yaliyopo hapo sebuleni.
“ngoja nimalizie
kupika shoga yangu.. nakuja sasa hivi.” Aliongea Miriam
“ngoja na mimi nije
jikoni nikusaidie shoga yangu.” Aliongea Jasmini na kunyanyuka.
“we kaa tu, mimi
namalizia. Nilianza kupika muda mrefu sana. Yaani hapa kila kitu kimeshaiva.
Naenda kumalizia tu hatua za mwisho.” Miriam aliongea hayo na kwenda jikoni
kuendela na mapishi yake.
“karibu sana
Jasmini.” Alikaribisha James na kumsogozea Jasmini rimonti zote alizokua nazo
pale karibu.
‘mimi naenda ndani
kujipumzisha kidogo. Kuwa huru Jasmini. Angalia kipindi ukipendacho na kama ni
mpenzi wa filamu basi kua huru kwenda kuchagua filamu uipendayo na kuangalia.”
Aliongea hayo James na kunyauka. Aliondoka na kumuacha mgeni huyo peke yake
sebuleni.
Baada ya kuiva kwa
vyakula vyote vilivyopikwa na Miriam. Alitenga kila kitu mezani na kweda
kumuamsha mume wake.
Hapo wakakaa pamoja
kwenye meza ya chakula na kupata chakula cha mchana.
Jasmini alishinda nyumbani
kwa rafiki yake mpaka jioni. Hapo ndipo alipoaga na kuondoka.
“kumbe shemeji mtu
poa sana… nilikua namuogopa nilivyomuona kwa mara ya kwanza.” Aliongea Jasmini
wakati walipokua njiani yeye na rafiki yake Miriam.
“ndio hivyo… usipotee
tena siku nyingine, ukishuka gari hapa unafika nyumbani ukinyoosha tu hii
barabara moja kwa moja.” Aliongea Miriam na kumuonyeshea njia Jasmini.
“yaani wewe unataka
niwe nakuja kwako tu, mbona huniambii ni lini utakuja kwetu?” aliuliza Yasmini.
“nitakuja jumamosi
ijayo… nakuahidi.” Aliongea Miriam na wakati huo huo daladala ikawa imeshafika.
“bye mpenzi…
tutaonana jumamosi kama kweli utakuja.” Aliongea Yasmini na kupanda gari hiyo
na ndipo Miriam alipoonyesha mkono ishara ya kumuaga rafiki yake na kurudi
nyumbani.
Maisha ya ubabe na
maamuzi ya upande mmoja ndio aliyotakiwa kuyazoea Miriam pindi atakapo amani na
mume wake. James hakua na muda maalumu wa kurudi nyumbani. Na anaporudi pia
hahitaji maswali juu ya wapi alikuwepo.
Ilimlazimu Miriam
avumilie tu na aone ni hali ya kawaida japokua kuna muda alikua akiumia moyo
hasa akisikia tetesi za mume wake kutembea na wadada wanaoanya kazi bar.
Starehe ya James ni
pombe. Na mara nyingi akilewa hulala nje ya nyumba au kurudi usiku ukiwa
umeshasogea sana.
Siku moja James
alikua kwenye moja ya Bar kubwa kinondoni mida ya saa kumi na moja jioni.
Ilikua ni bar ambayo hajawahi kwenda kunywa hata siku moja. Sema alivutiwa tu
mandhari ya bar hiyo na jinsi ilivyochangamka.
Alitulia na kuangalia
sehemu nzuri na kukaa huku akiliweka gazeti lake alilolinunua kwenye meza.
“nikuhudumie nini?”
aliuliza muhudumu mmoja aliyefika hapo kumuhudumia.
“niletee maji ya
Kilimanjaro makubwa.” Aliongea James na muhudumu huyo aliondoa na kurudi na
maji hayo. Baada ya kumuwekea kwenye meza, muhudumu uyo aliendelea kuwahudumia
wateja wengine.
Akiwa anakunywa maji
yae taratibu, ndipo kwa mbali alipoweza kumuona Jasmini akiwa na marafiki zake
wawili wakike wakipiga story na kunywa Savana. Alinyanyuka na kuwasogelea.
“habari warembo!”
Alisalima na
kuwafanya wote wamgeukie. Jasmini alimkumbuka na kumsalimia. Kwakua James
alikua sio mkubwa sana. Wote walimpa salamu ya vijana na kumfanya James
atabasamu.
“naweza kukaa hapa.
Au nitawatibulia story zenu?” aliuliza James na kuwafanya wasichana hao
watabasamu.
“karibu tu shemeji..
wala hakuna cha maana hapa tunachoongea zaidi ya kufurahi tu na kula
mishikaki.” Aliongea Jasmini na kumfanya James avute kiti na kukaa.
“mlikua mnahudumiwa
na nani?” aliuliza James.
“na Yule dada pale.”
Jasmini aliomuonyesha Yule muhudumu aliyemuhudumia hata yeye.
James alimuita ana
kuomba apigiwe hesabu zote walizokunywa hao wasichana pamoja na maji
waliyoagiza.
“jumla ni elfu kumi
na nane na mia tano.” Alijibu msichana huyo baada ya kuangalia karatasi yake.
“haya.. hii tunalipa
bili za nyuma. Kwa sasa tunaanza upya na chenji utakunywa soda na wewe.”
Aliongea James na kulipia kiasi cha shilingi elfu ishirini.
“ahsante sana.”
Aliongea msichana huyo na kutabsamu.
‘kuweni huru… kama
mnakunywa chochote ruhusa ya kuagiza nimetoa.” Aliongea James na kuwafanya
wasichana hao waliokua wanakunywa savanna zao huku wakilambalamba kama walikua
wakizibembeleza zisiishe mapema.
“niitieni mtu wa
nyama. Naona pamepooza hapa.” Aliongea James na mtu wa jikoni akaitwa kwenye
meza hio.
“nichomee miguu
miwili ya mbuzi na mishikaki hamsini… fanya haraka uje na bili yako kabisa
nikulipe.” Alingea hayo James na mtu wa jikoni akaitikia na kwenda kuandaa hiyo
oda.
“shemeji kula nyama,
kula bia. Usiogope ukiwa na mimi shemeji yako wa ukweli.”
Aliongea James baada
ya kilevi kuanza kumkolea. Hata Jasmini nae alianza kulewa na hao rafiki zake
waliokua wakizifakamia pombe ndio walipunguza spidi ya kunywa huku wakijitahidi
kwenda chooni ili kupunguza hali ya kimea kilichokua kikiwapanda kila dakika.
Walikaa mpaka saa nne
usiku. James aliteketeza kiasi cha shilingi laki sita pale pale na kuwafanya
wadada waliokua wanakunywa pombe kuzidiwa kabisa na mmoja wapo akazima pale
pale.
“shemeji utaweza
kuondoka kweli au niwatafutie chumba mlale?” aliuliza James kwa sauti ya kilevi
na isiyokua na aibu hata kidogo.
“ Mi siwezi kwenda
nyumbani, wewe nifanyie tu mpango wa chumba ili niweze kupumzika.” Aliongea
hayo Jasmini na kumfanya James aende conter na kulipia chumba kwa ajili ya
wasichana hao.
Yeye alijitahidi
kujikokota mpaka kituo cha kukodi taksi na kurudi nyumbani kwake.
Miriam hakua na
shida, bali furaha yake ni kushuhudia mume wake kua ameruudi salama bila kujali
amerudi saa ngapi.
Palipokucha asubuhi,
alienda bar kukata kilevi alichokua nacho na kuitazama simu yake. Aligundua kua
kuna missed call ya Jasmini. Alikumbuka kua alimpa namba yake na Jasmini
alimbipu. Ndipo alipojaribu kumpigia ili kumjulia hali.
“niambie shemu lake.”
Aliongea James baada ya Jasmine kupokea simu yake.
“yaani shemeji wewe,
umenifanya mpaka muda huu naona mia mia tu hapa.” Aliongea Jasmini na kulegeza
sauti hadi mwisho kutokana na uchovu aliokua nao.
“usijali, we kunywa
supu na soda, hicho kimea kilichopo kichwani kwako kitaondoka chote.” Aliongea
James na kumfanya Jasmine atabasamu.
“shemeji unaweza kuja
asubuhi hii?... au umebanwa?” allulza Jasmini swali la mitego na kumfanya James
atabsamu.
“sisi tunavyoishi
hakuna wa kumbana mwenzie. Nahisi ndio maana hatugombani. Hivyo wewe niambie
unahitaji nifike hapo saa ngapi. Maana asubuhi inaisha saa tano huko.” Aliongea
James.
“ukija muda huu
nitafurahi sana shemeji yangu.” Aliongea Jasmini huku akiwa amezidi kuilegeza
sauti yake na kuwa ya kudeka zaidi.
ITAENDELEA……….
RUDI 02
HUSSEIN O. MOLITO
“kwa hiyo ulitaka nije kulala nao hapa ndani…
si ndio?” aliongea James na kumtazama mke wake kwa dharau kasha akaondoka.
“naondoka. Nitarudi
nikijisikia. Na ukiongea naondoka tena. Mpaka uache huo mdomo wako. Pumbavu
kabisa wewe.” Aliongea James na kuondoka zake.
Hali iliyomfanya
mwanamke huyo mkjamzito aka echini ya kochi na kuamua kuangua kilia huku machzi
yakilowanisha mashavu yake.
Siku hiyo ilipita
tena bila James kurudi nyumbani. Alliirudi siku inayofuata huku akiwa amelewa
chakari. Aligonga mlango kwa fujo huku akimtukana Miriam
Miriam alienda
kufungua mlango na kumshuhudia mume wake akiingia ndani huku akipepesuka na
kwenda kujilaza kitandani.
Kwakua hakuhitaji
tena matatizo, alienda kumvua viatu na kuviweka mahala pake. Aliandaa chai na
kuitenga mezani kisha yeye mwenyewe kutoa nguo na kuanza kuzifua.
Baada ya James
kuamka. Alienda kunywa chai na kutoka nje. Hakumuongelesha kitu chochote Miriam
zaidi ya kumuangalia tu na kutoka huku kimea kilichokua kichwani mwake kikiendelea
kumtesa.
Baada ya james kutoka
nyumbani kwake, alienda moja kwa moja mpaka Bar na kulazimika kupata supu na
soda ili aweze kukata kilevi alichojitwika usiku kucha.
“nakuona bosi.. fanya
basi na mimi nishtue tumbo.” Ilisikika sauti ya msichana mmoja ambaye ni
muhudumu kwenye bar hiyo.
“unataka kunywa nini
mrembo?” aliuliza James huku anatabasamu
“mimi ninunulie tu
supu kama hiyo unayokunywa wewe.” Aliongea muhudumu huyo na kumfannya James
aingize mkono wake mfukoni na kutoa noti ya shilingi elfu kumi.
Lipia bili yangu ya
supu na bili yako. Kisha chenji utabaki nayo.” Aliongea hayo Jmaes na kumfanya
muhudumu huyo afurahi sana na kumshukuru.
Baada ya kupata supu
na soda baridi. Ndipo alipoanza kujisikia vizuri na kurudi nyumbani kwake.
Alimkuta mke wake
akimalizia kufua na kumpita tena bila kuongea naye kitu chochote. Alienda
sebuleni na kuwasha Televisheni. Alichukua rimonti ya king’amuzi na kuweka
stesheni aipendayo.
Baada ya Miriam
kumaliza kufua. Alirudi ndani na kumfuata mume wake kwa upole kabisa.
“nikupikie chakula
gani mume wangu?” aliuliza Miriam kwa sauti ya upole na kumfanya James
amuangalie.
‘kumbe adabu unayo…
pika ugali na samaki.” Aliongea James na kuingiza mkono mfukoni na kumpatia mke
wake noti ya shilingi elfu kumi.
Miriam alitoka na
kwenda kununua samaki . huko njiani ndipo alipokutana na msichana ambaye
walikua wanasoma wote shule moja kipindi alipokua sekondari.
“Miriam, hata
siamini. Umekua mdada mwenyewe mpaka umeamua na kuzaa kabisa.” Aliongea
msichana huyo huku akiwa na furaha ya kuonana na Miriam.
“si unajua maisha tu
Jasmini. Mii mwenywe natamani sana ningekua shuleni kama wewe.” Aliongea
Miriam.
“vipi, unaishi na
shemeji au ndio wale wale baada ya kutia mimba wanatoka mbio?” Aliongea Jasmini
na kumfanya Miriam atabasamu.
“mama nifungie
haraka… nachelewa.” Aliongea Miriam na kumuharakisha muuza samaki baada ya
kumpa maagizo na kumlipa kiasi cha fedha kulingana na mahitaji aliyochukua kwa
muuza samaki huyo anayemiliki na genge pia.
“twende kwangu
mpenzi, angalau ukatie hata Baraka.” Alongea Miriam.
“nitakuja siku
nyingine nyonyo… leo nimechelea vipindi. Halafu sio vizuri shemeji akiniona na
hizi sare za shule.” Aliongea Jasmini na kuonekana kukataa kabisa kwenda kwa
Miriam akiwa na sare za shule.
“na mimi ningekua
kidato cha sita kama wewe mwenzangu. Huu ukahaba huu umenifelisha mambo yangu
yote na mipango yangu yote imeyeyuka.” Aliongea Miriam na kuonyesha dhahiri kua
anajuta kukubali kuolewa na mvulana huyo ambaye hataki tena kusikia mambo ya
shule.
“usiseme hivyo..
maadamu umepata mtu wa kukusitiri basi shoga yangu tulia.” Aliongea Yasmini na
kumfanya Miriam atabasamu.
“ngoja nikapike mie.
Chukua basi namba yangu. Utanitafuta ukipta nafasai. Maana sipati picha
ulivyokutana na machizi wapya huko shuleni.” Aliongea Miriam na kumfanya
Jasmini acheke.
“yaani… huku kuna
machizi hata mimi mwenyewe naomba poo. Halafu katika kundi letu ni mimi peke
yangu ndio sina mimba. Wengi wana watoto na wengine wana mimba kama wewe. Ila
wengi wamekimbiwa na wengine waliozaa wamewaongezea mizigo wazazi wao. Sasa
ninachokushauri wewe tulia ili familia yako iishi kwenye mstari ulionyooka.”
Aliongea Jasmini na kuomba peni dukani na kuandika namba ya Miriam.
“nitakupigia usiku wa
leo nikirudi tu nyumbani. Nadhani jumamosi nitakuja nyumbani kwako. Unipikie
mahanjumati na mahanjamu mama kijacho.” Aliongea Jasmini na kuondoka huku
wawili hao kila mmoja akiwa amejawa na tabsamu.
Miriam alirudi
nyumbani na kumuandalia mume wake chakula anachokipenda na kutenga mezani.
Walikula kwa pamoja huku MMiriam akiuchunga mdomo wake asije kuulizia habari a
mume wake kuanz a kulala nje ya nyumba hiyo.
Usiku walilala
pamoja. Lakini James hakupitiwa na usingizi mapema kutokana na kuwa bize na
simu yake. Muda wote alikua akiichezea na kuchat na watu mbali mbali.
Huo ndio ulikua
ugomvi wa kwanza wa Miriam na mumewe. Lakini mwisho wa siku alizoea na ndio
ikawa kawaida kwa mume wake kuchati na watu mbali mbali mpaka muda ambao hata
Miriam hajui kutokana na kupitiwa na usingizi.
Palipokucha, mume
wake aliacha hela mezani na kutoka kwenda kwenye ofisi yake anayomiliki yeye
mwenyewe ndio maana anaenda muda anaotaka kwakua wafanya kazi walikua wanatosha
kuhudumia watu hata kama yeye asipokuwepo.
Jiioni ya siku hiyo
Miriam alipigiwa simu na rafiki yake na ikawa sababu ya yeye kuiihifadhi namba
ya Jasmini kwenye kitabu chake cha majina ya simu yaliyokua kwenye simu yake.
Siku ya jumaamosi,
alipigiwa simu na Jasmini na kumpa taarifa juu ya ugeni wake. Miriam
alijitahidi na kupia pilau la kuku. Na upande wa pili akaivisha wali wa maua.
Alianda rosti la maini na kufanya aamini kua mgeni wake atakifurahia sana
chakula hicho.
Alipata amani baada
ya simu yake kuita na kutokea jina la rafiki yake kwenye kioo cha simu yake.
“nipo hapa
tulipokutana siku ile.” Aliongea Jasmini na kumfanya Miriam amuambie asubri
hapo kwa dakka mbili tu.
Alimfuata mgeni wake
na kurudi nae nyumbani. Alimtambulisha rafiki yae huyo kwa James. Maana siku
hiyo James alipendelea kutulia nyumbani. Na hata kama akitaka kunywa basi
huijaza friji vinywaji mbali mbali hivyo kumfanya asitamani kutoka kabisa.
“huyu ni rafiki yangu
toka kidato cha kwanza… anaitwa Jasmin. Jasmin. Huyu ndio baba kijacho wangu.”
Alitambulisha Miriam na kumfanya Jasmin ampe mkono James.
Kwa james ilikua ni
kitu kingine kabisa baada ya kuruhsiwa kuushika mkono mlaini kabisa wa Jasmini
huku tabasamu alilliachia likimfanya James ahamie dunia nyingie. Hakumuachia
haraka hadi pale Jasmini alipotumia nguvu kidogo kuutoa mkono wake na kumfanya
James kurudisha network zake zilizopotea kwa sekunde kadhaa baada ya kushikana
tu mikono na kuangaliaa usoni.
ITAENDELEA…..
RUDI 01
HUSSEIN O. MOLITO
Alarm iliyotegeshwa
mida ya saa kumi na moja kamili ilianza kulia kwa fujo baada ya muda husika
kufika. Kwa uchovu kabisa kutokana na kuchelewa kulala siku iliyopita, ZABRON
aliamua kulitupa shuka pembeni na kuizima saa yake hiyo iliyokua ikitoa mlio
mkali.
Alipapasa kwenye meza
na kuchukua kibiriti. Alichukua njiti moja na kukiwasha kibiriti hicho
kilicholeta mwanga hafifu na kumfanya aweze kuiona kandili yake iliyokua kwenye
meza hiyo iliyokua mita moja tu kutoka kwenye usawa wake wa kitanda.
Baada ya kuiwasha
kandili hiyo. Aliufuata mswaki wake na kuuweka mdomoni bila kujali kama bado
hajaweka dawa ya meno kwenye mswaki wake. Hilo alilifanya kwakua tu alikua
anafahamu kua hiyo dawa ya meno alikua ameitumia kwa mara ya mwisho miezi
miwili iliyopita na hakua na bajeti ya kuinunua tena kwa wakati huo.
Alimimina maji nusu
kenye ndoo yake a kuufungua mlango wake a kutoka nje. Baada ya kuvaa ndala
zake, alihesabuhatua kama ishirini na ndipo alipokfikia choo na bafu ambavyo
vyote vipo sehemu moja.
Baada ya kumaliza
kuoga, alirudi ndani na kujiandaa tayari kw ajili ya kwenda kusaka riziki.
Kwakua Mabibo bonde
la mchicha sio mbali sana na kiwanda cha Vitenge na Khanga cha NIDA sio mbali
sana na anapoishi, basi ilikua ni kazi yake kutembea kwa mguu hadi kazini
kwake. Ilikua inamchukua mwendowa nusu saa au dakika arobaini sik nyingine.
Alifika kiwandani
hapo na kukutana na wenzake wengi ambao alikua wanasubiri muda w akuingia
ufike.
Walitwa kwa majina na
kuingia huku wakiwaacha vibarua wengine wakiwa nje baada ya kukosa nafasi
kutokana na idadi ya wafanyakazi waliokua wakihitajika siku hiyo.
Baada ya kupiga kazi
kwa masaa nane. Ndipo alipopokea ujira wake ambao ni shilingi elfu nne na mia
tano. Akatoka na kwenda kwa mama muuza chakula na kununua chakula cha shilingi
elfu moja na mia mbili na kushushia na maji ya kufunga mawili.
Kwa kila siku alikua
akihakikisa anarudi na shilingi elfu tatu nyumbani. Hivyo mara zote Zabron hua
hanywi chai. Anasubiri chakula cha mchana na ndipo anapozitibu njaa zote
alizokua nazo. Hata chakula hua anapendelea makoko au matandu, kwa maana watu
wanaokula vyakula hivyo vya chini huwekewa ujazo mkubwa kuliko chakula
kilichokua kwenye hali ya kawaida.
Baada ya kufika
nyumbani. Ndipo alipoamua kujipumzisha ili kupuguza uchovu aliokua nao.
Ilipofika saa kumi na
moja na nusu, Zabron aliamka na kwenda uwanjani kutazama mpira. Alirudi
nyumbani kwake saa kumi na mbili na nusu na ndipo alipoenda kuoga kwa mara
nyingie ili apate akili mpya.
Mbali na kufanya kazi
kiwandani. Zabron ana ndoto nyingi. Moja wapo kuja kuwa muandishi mkubwa sana
wa vitabu vya riwaya, tamthilia na mashairi.
Alinunua daftari lake
kubwa kabisa na kuanza kuandika story moja ya hisia aliyoitunga kichwani mwake.
Mara nyingi hua
anaandika karatasi sita mpaka saba ndio anaridhika. Maana hutumia muda wa masaa
mawili mpaka matatu kutimiza karatasi hizo na ndipo anapotoka na kwenda
kutafuta chakula ambacho hununua kwa shilingi elfu moja na kumfanya awe na
uwezo wa kuhifadhi shilingi elfu mbili kwa siku.
Maisha yalikua ni ya
kawaida kwake kwakua alishayazoea. Na hakuonekana kusononeka kwakua alikua na
uwezo wa kulipa kodi ya chumba bila maatizo yoyote yale. Kubwa zaidi
anachoshukuru ni kwamba, kazini kwao alikua anategemewa sana. Hivyo alikua na
uhakika wa kuingia kila siku na sio wengine ambao mara nyingi walikua wanapenda
kuingia lakini siku nyingine wanakosa nafasi iwapo watahitajika wafanyakazi wa
chache kwa siku hiyo.
Hayo ndio maisha ya
Zabron. Na mara zote kwake huwa ni furaha kwenda kazini siku za sikukuu. Maana
huwa wanalipwa elfu kumi na kumfanya afurahie zaidi kuwepo kazini siku za
sikukkuu kuliko kubaki nyumbnani.
Hakuwahi kuwa na
mwanamke katika maisha yake. Maana aliwahi kuanza kujitegemea na baadae kuwa
mlezi akiwa na umri wa miaka kumi pekee.
Alisoma shule ya
awali na msingi ambapo hakufanikiwa kufika hata darasa la saba. Aliacha shule
akiwa darasa la tatu pekee baada ya nguzo ya familia kuteketea.
Zabron alianza
kusimama kama baba akiwa na umri wa miaka kumi huku akitakiwa kumuuguza mama
yake mzazi ambaye alikua kiugua virusi vya Ukimwi.
Ndugu wote
waliwatenga hasa baada ya kumshutumu mama yake Zabron kua ndio aliyemuambukiza
baba yake ugonjwa huo.
Ukweli juu ya maisha
ya mama yake Zabron alikua akiujua Zabron japo alikua na umri wa miaka sita
pekee. Hata shule ni mama yake ndio alikubali kupigwa na baba yake ili mradi
aweze kupata elimu. Japo hakupata elimu kubwa, lakini daima anamuombea mama
yake alazwe mahala pema peponi baada ya kumsaidia angalau akajua hata kusoma na
kuandika.
“mwanangu. Najau umri
wako bado mdogo sana na kuna uwezekano ukashindwa kuhimili haya mazito
nitakayokuelezea. Ila amini kuwa wazazi wako tuna miaka michache sana ya
kuishi. Nakuomba usome kwa bidii ili aweze kuyaokoa maisha yako kwenye
ulimwengu huu ambao tutakuacha. Huo ulimwengu hautakua na ndugu wala rafiki
atakaye kuthamini. Ulimwengu ambao unatakiwa ujishike mwenyewe na utakapopata
bahati ya kubebwa basi jishikilie vizuri na uwe mstaarabu ili usimkere huyu
ambaye ataamua kukubeba na kukufikisha mahali. Nakuambia soma kwakua mwisho
wako naujua mwanangu. Niombee maisha marefu. Angalau miaka kumi mbele. Pengine
utaweza hata kufika la saba na kufuta ujinga. Najua unajua kua baba yako hawezi
kukusomesha na hataki kusikia habari za shule ya awali. Lakin mimi nitakupeleka
na ujitahidi kumsikiliza mwalimu ili mwakani ukaanze la kwanza.”
Hayo yalikua ni
maneno ya mama yake Zabron akimuambia mtoto wake pindi alipofikisha umri wa
miaka sita pekee.
Yalikua ni maneno
yasiyokua na uzito moyoni wa Zabron kwa wakati huo. Lakini kumbukumbu ya maneno
hayo yalikua yamepokelewa vizuri kwenye ubongo utunzao kumbukumbu. Kwani kila
anavyozidi kukua ndipo maana halisi ya kile alichokua akiambiwa kilikuja na
kujirudia katika ubongo wake. Ndipo kila tamshi la mama yake alipoliona lina
ukweli ndani yake.
“ulazwe mahala pema
peponi mama.”
Alijikuta akiongea
hayo kila akiyapitia mazito ambayo mama yake alishamtabiria akiwa na umri mdogo
kabisa.
********
“nimekuambiaje,
ukitaka kujua nikiwa na hasira hua nakuwaje, basi endelea kuniuliza maswali ya kijinga.”
Aliongea baba mmoja kwa hasira huku akimfokea mke wake ambaye nae alionekana
kua na hasira pia.
“hapana James, leo
utaniambia tu jana umelala wapi?” aliongea mwanamke huyo mjamzito na kumfanya
James amuangalie na kumshika mikono yake kwa nguu.
“isingekua hii mimba
ningeshakuvuruga sasa hivi. Mimi mwanaume ndani ya hii nyumba. Mwanaume
haulizwi ulikua wapi au unatoka wapi. Mwanaume anapokewa alichokileta kisha
ndio kwa utaratibu unahoji na sio kuropoka na kupaza sauti tu. Hivi hujafundwa
wewe huko kwenu jinsi ya kumpokea mwanaume pindi akichelewa kurudi?.. unakua
kama umezaliwa shimoni bwana.” Aliongea James na kuiachia mikono ya mke wake.
“James leo
unanitusi?” aliuliza mwanamke huyo kwa hasira.
“usinipigie kelele
wewe mwanamke. Maana ukiendelea kuongea nitaondoka tena.” Aliongea James na
kwenda kukaa kwenye kiti.
“mimi leo hata
sikubali.. liwalo na liwe.” Aliongea mwanamke huyo na kumfuata mpaka pale James
alipokaa.
“naomba niambie ni
wapi ulipoenda kulala jana.. yaani James mbali na visa unavyonifanyia, bado
unaamua kulala na wanawake zako huko nje kweli?” aliuliza Mwanamke huyo huku
machozi yanamtoka.
“kwa hiyo ulitaka
nije kulala nao hapa ndani… si ndio?” aliongea James na kumtazama mke wake kwa
dharau kisha akanyanyuka.
“naondoka. Nitarudi
nikijisikia. Na ukiongea naondoka tena. Mpaka uache huo mdomo wako. Pumbavu
kabisa wewe.” Aliongea James na kuondoka zake.
Hali iliyomfanya
mwanamke huyo mjamzito akae chini ya kochi na kuamua kuangua kilio huku machozi
yakilowanisha mashavu yake.
ITAENDELEA…………..
USIWAELEZE WATU SHIDA ZAKO, KWA SABABU:-
1. 3/4 (ROBO TATU) YA UTAOWAAMBIA HAWATAKUSIKILIZA
2. 1/2 (NUSU) YA UTAOWAAMBIA WATAKUCHEKA
3. 2/3 (THELUTHI MBILI) YA UTAKAO WAAMBIA NAO WAKO NA
SHIDA KAMA WEWE!!!!
HIVYO CHUNGA SANA KINYWA CHAKO JUU YA MABO YAKO:
VITUKO MASHULENI:
Mwalimu katoa kazi kwa watoto, kila mmoja atunge sentensi kutokana na maneno yafuatayo;
- TUMAINI
- SUKARI
Mwanafunzi:
1.SENTENSI: TUMAINI TWA MBUZI NI TUTAMU KULIKO TWA NG'OMBE
Mwanafunzi:
2. SENTENSI: NILIKUNYWA CHAI ASUBUHI NA MAPEMA SANA:
Mwalimu: SASA NENO SUKARI LIKO WAPII??
Mwanafunzi: SUKARI IMO NDANI YA CHAI, MWL UTAKUNYWAJE CHAI BILA SUKARI KWELI INAWEZEKANA:
Christmas
C is for Christmas I wait for all year.
H is for holly that brings so much cheer.
R is for reindeer that pull Santa's sleigh
I is for icicles dripping all day.
S is for Santa who seldom is seen.
T is for tree that is lovely and green.
M is for mistletoe, hugs and a kiss.
A is for angel who looks just like this.
S is for stockings all loaded with toys
From all of the elves to the girls and the boys.
Christmas Time (Farmer in the Dell)
Christmas time is here
Christmas time is here
Hustle bustle busy time
As Christmas time is here
Christmas trees are up
Christmas trees are up
Tinsel balls and popcorn too
As Christmas time is here
Santa Claus is here
Santa Claus is here
Bringing gifts and stockings too
As Christmas time is here
Christmas time is a beautiful time
With lights all red and green,
I think it is the prettiest time
That I have ever seen!
Christmas Acrostic (may be used for a concert)
C - is for the Christ child born upon this day
H - is for the holly to make our mantle gay.
R - is for red ribbon to wrap the parcels tight
I - is for the icicles On this cold winter night.
S - is for dear Santa Please leave him a treat
T - is for the turkey It is so good to eat.
M - is for the manger Where Baby Jesus lay,
A - is for the angels On that first Christmas Day.
S - is for the stockings Hanging in a row With candy canes out of the top and bulges in the toe.
Isn't it strange?
• Isn't it strange how a 20 dollar bill Seems like such a large amount when You donate it to church, but such a Small amount when you go shopping?
Isn't
it strange?
•Isn't
it strange how 2 hours seem so long when you're at church, and how short they
seem when you're watching a good movie?
Isn't
it strange?
•Isn't it strange that you can't find a word to
say when you're praying, but you have no trouble thinking what to talk about
with a friend?
Isn't
it strange?
•Isn't
it strange how difficult and boring it is to read one chapter of the Bible, but
how easy it is to read 100 pages of a popular novel?
Isn't
it strange?
•
Isn't it strange how everyone wants front - row - tickets to concerts or games,
but they do whatever is possible to sit at the last row in Church?
• Isn't it strange how we need to know about an event for Church 2 - 3 weeks before the day so we can include it in our agenda, but we can adjust it for other events in the last minute?
Isn't
it strange?
• Isn't it strange how difficult it is to learn a fact about God to share it with others, but how easy it is to learn, understand, extend and repeat gossip?
• Isn't it strange how difficult it is to learn a fact about God to share it with others, but how easy it is to learn, understand, extend and repeat gossip?
Isn't
it strange?
•
Isn't it strange how we believe everything that magazines and newspapers say,
but we question the words in the Bible?
Isn't
it strange?
• Isn't it strange how everyone wants a place in heaven, but they don't want to believe, do, or say anything to get there?
• Isn't it strange how everyone wants a place in heaven, but they don't want to believe, do, or say anything to get there?
Isn't
it strange?
• Isn't it strange how we send jokes in e - mails and they are forwarded right away, but when we are going to send messages about God, we think about it twice before we share it with others?
• Isn't it strange how we send jokes in e - mails and they are forwarded right away, but when we are going to send messages about God, we think about it twice before we share it with others?
Isn't
it strange?
• IT'S STRANGE ISN'T IT?
Now that you've read this message, forward it to anybody that you consider a friend. If you don't do it, not only you will deprive yourself from being blessed, but you will also do that to others who may need God in their life.
• IT'S STRANGE ISN'T IT?
Now that you've read this message, forward it to anybody that you consider a friend. If you don't do it, not only you will deprive yourself from being blessed, but you will also do that to others who may need God in their life.
YES, IT IS STRANGE …
GOD BLESS YOU !!!!!!!!!!!!
If your boss comes to you and says:
There will be no salary increases for this year ………..
There are no bonuses either ……… All overtime has been cancelled No expenses will be paid.....
And there will be no additional healthcare !
What
will your reaction be ? …………………….!!
No comments:
Post a Comment