BIASHARA YA KIFO
Sehemu ya 04
Hakukuwa na kitu
alichokifikiria zaidi ya ngono, alitaka kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza
katika maisha yake, hakutaka kumuacha Irakoze hivihivi, alitaka kuhakikisha
kwamba kibaridi kile kilichokuwa kikipiga, ni lazima kikatishwe na joto la
mwili wa Irakoze.
Alitembea kwa
harakaharaka kama mtu aliyekuwa akiwahi kitu fulani, alipofika ndani, akasikia
maji yakimwagika bafuni, akajua ni lazima Irakoze alikuwa ndani ya bafu lile
akioga. Hakutaka kujiuliza, akausukuma mlango, ukafunguka, naye akazama ndani.
“Aaaah! Padri!”
alisema Irakoze huku akijifanya kujificha.
“Usiogope.”
“Naoga padri, naomba
uende nje,” alisema Irakoze.
Hiyo ilikuwa ni sawa
na kumpigia mbuzi gitaa acheze, padri Benedicto hakutaka kutoka, alichokifanya
ni kuusukuma mlango na kubaki humohumo. Kwa sababu naye mwenyewe alikuwa
akimpenda sana padri huyo kutokana na uzuri wa sura yake, hakutaka kuiacha
nafasi hiyo, akaitumia vilivyo na hivyo kujikuta wakigusana miili yao, maji ya
bomba la mvua yaliwamwagikia, walipapasana hapa na pale na hatimaye kufanya
dhambi.
Huo ndiyo ukawa
mwanzo wa kila kitu, mchezo walioufanya siku hiyo ukampelekea hata Irakoze
kuhama chumba chake na kuhamia kwa padri huyo. Waliishi kama mume na mke,
hakukuwa na mtu yeyote nje ya nyumba hiyo aliyefahamu kile kilichokuwa
kikiendelea.
Ilikuwa siri kubwa
mno, na kila alipotoka nyumbani, padri Benedicto alijifanya kuwa mtakatifu mno,
kumbe jana yake tu alikuwa amelala na Irakoze usiku mzima.
“Tumsifu Yesu
Kristo!” alisema padri yule.
“Milele Amina.”
Usiri mkubwa
uliendelea, padri Benedicto hakutaka kuonekana kuwa rahisi kwa wanawake wengine
ambao walimfuata kwa kisingizio cha kutaka kumwagiwa maji ya baraka kumbe upande
wa pili walikuwa wakihitaji kulala naye.
Mwanamke aliyekuwa
naye nyumbani, alimtosheleza na hata alipokuwa akifuatiliwa na wanawake
wengine, hakutaka kuwakubalia kwa kisingizio kwamba alikuwa mtu wa Mungu na
hakutakiwa kuoa kutokana na cheo alichokuwa nacho.
“Ninakupenda mpenzi,”
alisema Irakoze.
“Nakupenda pia!”
“Hivi siku ikitokea
nikapata mimba?”
“Utapataje?
Haiwezekani, tupo makini kila siku, wala usijali, mimba haiwezi kutokea,”
alisema padri Benedicto.
Hakukuwa na aliyejali
sana, padri Benedicto alikuwa na uhakika kwamba kila kitu ambacho kiliendelea
kamwe asingeweza kumpa mimba msichana huyo. Siri kubwa iliendelea, waliishi
kama mume na mke.
Wakati mwingine padri
Benedicto hakuwa akielekea kanisani, alibaki nyumbani kwa ajili ya kufanya
mapenzi na msichana huyo tu. Japokuwa kila siku washirika walimtembelea padri
wao lakini hakukuwa na yeyote aliyefahamu kama watu hao walikuwa kwenye
uhusiano mkubwa wa kimapenzi.
Siku zikakatika,
miezi ikaendelea kukatika. Padri Benedicto akaingia moja kwa moja kwenye
ulimwengu wa kishetani, naye akaanza kwenda klabu usiku, akaanza kunywa pombe
kali zilizomfanya hata kutokuthamini kazi yake ya upadri.
Mabadiliko yale
yalimshangaza mno Irakoze, hakutaka kuzungumza naye sana kwa kuamini kwamba
mabadiliko hayo yangetokea kipindi hicho tu, cha kushangaza, hakuacha, kadiri
siku zilivyozidi kwenda mbele na ndivyo alivyozidi kubadilika.
Kila siku usiku,
akawa mtu wa kutoka na kwenda klabu, huko, alikuwa akivalia kofia kubwa ili
asijulikane na mtu yeyote. Alikunywa pombe na wakati mwingine kulewa mno,
maisha ya kidunia yakaanza kumteka kiasi kwamba wakati mwingine alipokuwa
akirudi nyumbani na kulewa, kesho yake hakwenda kabisa kanisani kwani kichwa
bado kilikuwa na pombe kali.
“Kuna kitu ninataka
kuzungumza nawe,” alisema Irakoze.
“Kitu gani?”
“Mbona
sikuelewielewi! Hebu tulia kwanza,” alisema msichana huyo.
“Nitulie kivipi tena?
Unajua leo lini?”
“Jumapili!”
“Basi subiri kwanza
niende kanisani,” alisema padri Benedicto.
Japokuwa Irakoze
alikuwa na jambo muhimu la kuzungumza na padri huyo lakini hakuweza kupata
nafasi hiyo. Ilikuwa ni Jumapili ya tatu tangu asitishe kwenda kanisani kwa
kisingizio cha kuwa bize kufuatilia mizigo iliyotumwa kutoka nchini Vatican kwa
maendeleo ya kanisa hilo.
Ingawa alikuwa
akidanganya kwa kujifanya mfuatiliaji namba moja lakini hakukuwa na mtu
aliyemshtukia kwamba ni pombe za janausiku ndizo zilizomuweka nyumbani na
kushindwa kabisa kwenda kanisani.
Siku hiyo alipanga
kwenda huko kwa ajili ya kuhubiri, alijua ni kwa jinsi gani washirika wake walikuwa
wamemkumbuka kwani katika kipindi chote alichokuwa akikaa nyumbani, alikuwa
akipigiwa simu na kuuliziwa maendeleo yake.
Siku hiyo
alipoonekana kanisani, kila mshirika alikuwa na furaha, wiki tatu ambazo
hakuonekana kabisani hapo zilionyesha kila dalili kwamba kanisa hilo lingepwaya
sana na hatimaye lingeweza kupotea kabisa.
Ujio wake ukaibua ari
ya washirika wake na hatimaye kuendelea na huduma kama kawaida. Kwa
kumwangalia, usingeweza kuamini kwamba jana usiku alishinda klabu ya muziki,
alionekana mchangamfu na hata macho yake hayakuonyesha kabisa kama alikuwa mtu
aliyekesha.
Japokuwa alikuwa
akihubiri na kuwabariki watu waliokuja na watoto wao kanisani hapo lakini mara
alipokumbuka kwamba Irakoze alitaka kuzungumza naye asubuhi ya siku hiyo,
ghafla amani ikakatika.
Hakukuwa na kitu
alichokiogopa kama kuambiwa kwamba mtu fulani alitaka kuzungumza naye. Hakujua
ni kitu gani kiliendelea lakini mwisho wa siku akataka kukaa chini na msichana
huyo ili kumsikia alikuwa na jambo lipi la kuzungumza.
Ibada ilipokwisha,
hakutaka kukaa kanisani na kuwasalimia washirika, alichokifanya ni kuondoka na
kuelekea nyumbani kwake. Alipofika huko, kama ilivyokuwa siku nyingine,
alipokelewa kwa mahaba mazito mpaka chumbani, hata kabla hajafanya lolote,
akavuliwa joho na kupigwa mabusu mfululizo, ndani ya dakika tatu tu, alibaki
kama alivyozaliwa.
Kilichofuata ni
kilekile kilichokuwa kikitokea siku zote, walifanya dhambi kwa takribani masaa
matatu na ndipo kila mmoja akaridhika na kutulia pembeni ya mwenzake.
“Aya niambie ulitaka
kuniambia nini asubuhi,” alisema padri Benedicto.
“Una moyo?”
“Ninao. Hebu niambie
wala usinitishe.”
“Usiogope, nafikiri
ni baraka kutoka kwa Mungu.”
“Ipi?”
“Nina mimba yako!”
“Unasemaje?” aliuliza
padri huku akionekana kushtuka.
“Nina mimba yako!”
Padri Benedicto
akasimama na kuanza kumwangalia Irakoze, hakuamini kile kilichokuwa
kimeongelewa maahali hapo, alimwangalia msichana yule, ndiyo kwanza alikuwa
akitabasamu kwa furaha, hakuonekana kujua ni kwa jinsi gani padri alijisikia
moyoni mwake.
Kama masharti ya
kanisa hilo, hawakutakiwa kuoa, si kuoa tu, hawakutakiwa kuwa na mtoto pia.
Kauli ya Irakoze ilimuweka katika wakati mgumu, mwili wake ukaanza
kutetemekea huku kijasho chembamba kikimtoka.
“Unasemaje?”
“Nina mimba yako!”
Alitamani jibu
libadilike na kuambiwa kwamba alikuwa akitaniwa, kile alichoambiwa sekunde
chache ziliopita kilikuwa kilekile alichoambiwa kwa mara nyigine tena,
akajikuta akitoka chumbani humo na kuelekea sebuleni.
“Kuna nini?” aliuliza
Irakoze.
“Hivi unajua misingi
ya kania letu?”
“Ndiyo! Ila mtoto ni
baraka mpenzi!”
“Haiwezekani! Mtoto
si baraka katika maisha yangu! “
Hakukuwa na kitu
kilichomchanganya katika maisha yake kama hicho, hakuamini kile kilichokuwa
kimetokea kwamba baada ya kufanya sana mapenzi mwisho wa siku msichana wake
alikuwa mjauzito.
Wakati mwingine
alifikiria kuikataa mimba hiyo ila kila alipona kwamba ndipo kungekuwa na
madhara zaidi kwa msichana huyo kutangaza, akaogopa. Kama ilivyokuwa siri
katika kipindi cha nyuma, ilitakiwa kuendelea kuwa siri maisha yake yote, iwe
isiwe, ilikuwa ni lazima kuhakikisha kwamba jambo hilo halijulikani na mtu
yeyote yule.
“Naomba tufanye kitu
ili unifiche na aibu hii,” alisema Padri Benedicto huku kijasho chembamba
kikianza kumtoka na mwili ukizidi kumtetemeka. Irakoze akamkazia macho.
INAENDELEA...
No comments:
Post a Comment