Sikia kisa cha
bwana mmoja ambaye alikuwa mkali sana kwa mke na watoto wake kwa ujumla,
Mkasa ulikuwa
hivi yule Bwana aliumwa kiasi cha kuzidiwa sana tu ndiko akapelekwa hospitali
na mkewe. Ndipo akatakiwa
afanyiwe uchunguzi wa kina kujua nini tatizo linalomsibu.
Daktari akamwambia
mkewe kua akalete mkojo toka kwa mumewe wapate mfanyia uchunguzi.Ndipo akaenda
akamweleza hilo swala naye mume hakusita akafanya hivyo na kumpatia mkewe huo
Mkojo apate
ufikisha kwa daktari, sasa wakati anatoka kwenda kwa daktari bahati mbaya
akajikwaa na hatimaye
kumwaga ule mkojo wote alokua akipeleka kwa daktari.