Sikia kisa cha
bwana mmoja ambaye alikuwa mkali sana kwa mke na watoto wake kwa ujumla,
Mkasa ulikuwa
hivi yule Bwana aliumwa kiasi cha kuzidiwa sana tu ndiko akapelekwa hospitali
na mkewe. Ndipo akatakiwa
afanyiwe uchunguzi wa kina kujua nini tatizo linalomsibu.
Daktari akamwambia
mkewe kua akalete mkojo toka kwa mumewe wapate mfanyia uchunguzi.Ndipo akaenda
akamweleza hilo swala naye mume hakusita akafanya hivyo na kumpatia mkewe huo
Mkojo apate
ufikisha kwa daktari, sasa wakati anatoka kwenda kwa daktari bahati mbaya
akajikwaa na hatimaye
kumwaga ule mkojo wote alokua akipeleka kwa daktari.
Akawaza moyoni mwake
Akawaza moyoni mwake
“kwa jinsi mume
wangu alivyo mkali ntamwambia nini sasa tena ukizingatia anaumwa “
Alichoamua ni
kwenda kuweka mkojo wake binafsi na
kumpelekea daktari kwa uchunguzi ili kuepuka ugomvi
na mumewe kisha akarudi kwa mgojwa ili wasubirie majibu toka kwa daktari.
Muda si mrefu
daktari akaingia kuwapatia majibu ndipo akaanza kwa kusema
“kutokana na
uchunguzi tulio ufanya kwa mgonjwa wetu, mgonjwa anaonekana kuwa ana Ujauzito wa miezi miwili". Mgonjwa akasema naomba rudia
kusema hayo majibu?.
Akamwambia vivyohivyo tena kuwa mgonjwa ana ujauzito wa miezi miwili, ndipo akaamua kuondoka na akawa amepona tokea hapo kutokana na majibu
yaliyo msitaajabisha toka kwa daktari.
USHAURI WA BURE
No comments:
Post a Comment