Saturday, 29 October 2016

HADITHI ZETU!!!

MTU ALIYEKUWA TAJIRI NA HAKUBAHATIKA KUPATA MTOTO WA KUMFAA

Imesimuliwa na Ngwali Mashaka
Hapo zamani za kale alikuwepo bwana mmoja aliyekuwa akiitwa Hassan Saira.  Bwana huyo alikuwa ni tajiri sana kwa wakati wake. Vile vile alikuwapo mtu mmoja katika kijiji hicho ambae ni masikini sana bwana huyo alikuwa akiitwa Bwana Vuai Pandu. Bwana Hassan ni mtu mmoja wapo aliyepewa uwezo mzuri na Mwenyezi Mungu.
 Bwana huyo alioa na akapata mtoto mmoja wa kiume aliyeitwa Maulid. Mtoto wake huyo alikuwa ni mgonjwa, lakini moyo wake ulipenda amuozeshe na huenda ikawa bahati nzuri akapoa na kupata mtoto ambaye aliweza kumfaa babu yake. Bwana Hassan alikwenda kwa jirani yake Bwana Vuai Pandu ambaye alikuwa na watoto wengi wake na waume. Bwana Hassan alikwenda kuposa katika nchi moja wapo ya kifalme na kumwambia mzee Vuai kuwa mtoto wangu nimemposea lakini ni mgonjwa haifai kuonekana. Lakini nimekuja kwako unipe mtoto wako mmoja aitwae Yunus. Bwana Vuai alisema na kumwambia Bwana Hassan mimi mtoto wangu ni masikini jee atawezaji kufika kutoka nchi hizo za kifalme na akaonekane kuwa ni mtu? Bwana Hassan alijibu kuwa ataonekana kuwa ni mtu, usijali.
 Bwana Vuai alimuelezea mkewe Bibi Khadija kadhia hiyo. Bi. Khadija alimwambia mumewe jee haitakuwa taabu baada ya kwishakuoana, kwa sababu kila mmoja atakuwa anampenda mwenziwe?  Mzee Vuai alisema si tatizo nitamnasihi sana baada ya kurudi hapa tu kuwa amwache. Hapo alimwambia asili ya kukwambia hayo sisi hapa ni masikini tusipokubali anaweza hata kutufukuza, tutafanya nini?  Kwa hiyo ni bora tukubali.  Baada ya maneno hayo Bi Khadija aliridhika na Bwana Vuai alipeleka jawabu kwa Bwana Hassan Saira kuwa ameridhika kumpa mtoto wake. Na hapo ilifanywa safari, akasafi ri kwa meli, huku mtoto wa Bwana Vuai akapambwa na kuonekana ni mtoto wa mfalme. Pia askari walichukuliwa wakenda kwenye harusi. Mizinga ilisikika siku ile ya kupokewa bwana harusi na kukaribishwa wapite ndani ya kasri ya Mfalme. Gari nyingi za watu zilikuja katika sherehe hiyo na mtoto wa mfalme akachukuliwa na kufanyiwa kama ilivyo ada ya harusi na wafalme wote waliohudhuria walifurahi sana kwa kupata mchumba mzuri wa kifalme.
Baada ya hapo ilifanyika safari ya kurudi nyumbani ambapo alikabidhiwa watumishi mbali mbali, wa kike na wanaume. Mizinga ya harusi ya kurudi ilisikika na watu wote walikuja kumpokea harusi. Shangwe na vigelegele vilizagaa mtaani kwa Bwana Hassan Saira. Na walipofi ka maharusi nyumbani kwao watu walikaa na kushereheka usiku wa kucha.  Ilipofi ka siku ya pili Bwana Vuai alikwenda kuomba kuonana na mwanawe Yunus. Yunus hakupinga amri ya mzee wake na hapo Yunus akamuaga mkewe kuwa anakwenda kuangalia bustani zake na alitoka nje kwa muda mchache na hatimayae mtoto wa mfalme akaletewa mume mwengine na kuambiwa huyu ndie mumeo. Bi harusi alisema huyu siye mume wangu niletewe mume wangu na hapo alilia kwa muda mrefu na kilio kilizagaa katika nyumba mpaka watu wote wakatetemeka.
Aliitwa Bwana Hassan na kuelezwa kuwa Bi harusi hataki lolote na anataka kurudi kwao au aletewe mume wake kwani aliyeletewa siye mumewe halisi. Bwana Hassan alipofi ka mabibi wa nyumbani walimwambia utuletee mume wetu kwa haraka. Si hivyo tunakwenda zetu.  Ikabidi Bwana Hassan kusema kuwa huyu ndiye mume wako lakini bibi harusi akasema aitwe baba yake mzazi.  Bwana Hassan alipeleka barua ya ugonjwa ili kumrudisha kwao kwa sababu tu hataki kukaa na mume aliyekuwa siye aliyeozeshwa.
Mfalme alipopata barua na kufi ka kule nyumbani aliletewa mwanawe. Baada ya kuzungumza na watu wa nyumbani alihisi kuwa hana sifa ya ugonjwa. Hivyo bwana mfalme aliandika barua ya kumshitaki Bwana Hassan kwa kitendo alichokifanya ambacho si cha ukweli. Bwana Hassan alishitakiwa na kutakiwa kulipa fi dia kwa kitendo alichokifanya cha kuozeshwa mtu mgonjwa .
Bwana Hassan alikubali na kulipa fedha pamoja na masharti yote aliyopewa. Baada ya hapo mtoto wa mfalme alimwambia mzee wake kuwa alifanya hadaa tu kumletea mtu mzima na baadae kupewa mbovu, kwa hivyo mimi ninamtaka yule niliyeozeshwa mwanzo. Nina hakika bado kijana yule hajafa katika nchi ile, hivyo nikaozeshwe yule yule na niletewe mwenyewe.
Kwa kweli mfalme alisononeka sana kwa kitendo hicho kwa sababu mtoto wake alikuwa hali wala halali. Mfalme alitoa askari na kwenda kwa Bwana Hassan Saira na kumtaka apewe yule kijana aliyekuja kumuozesha mwanawe na wampeleke kule aliko mwana wa mfalme. Hapo Bwana Hassan alikwenda kwa Bwana Vuai na kumwambia kuwa mfalme amekuja na anamtaka yule kijana wako tumpelekee.
Lakini Bwana Vuai alimwambia Bwana Hassan kuwa mwambie mfalme aje mwenyewe na asitume askari. Baada ya hayo askari walipeleka ujumbe na mfalme akaja kutokana na shida ya mwanawe. Mfalme baada ya kufi ka kwa Bwana Hassan, akapelekwa kwa Bwana Vuai Pandu.  Bwana Vuai alitakiwa kumwita mtoto wake ili waende pamoja.  Walipofi ka alisema; „nasikia umetuma ujumbe kuwa nije mwenyewe nisitumize mtu yeyote, kwa hivyo tayari nimekwishafi ka.” Hapo Bwana Vuai alisema huyu ndie mtoto wangu alichukuliwa kwa hadaa ili kuozeshwa mtoto wako. „Jee wewe ukiangalia anastahiki kuchukuliwa kuja huko?”
„Unakuja kuchukua mtoto wangu, kutokana na umasikini tulio nao hebu twende ukaangalie nyumba yetu ilivyo tunavyoishi,” alisema. Mfalme alikubali hayo yote na baada ya kufi ka aliona nyumba yao na alimwambia warudi tena kwa Bwana Hassan. Na baada ya kufi ka aliamrisha aletewe yule motto aliyekuwa mgonjwa, kwa kweli mfalme alisikitika sana baada ya kuona hali yake. Baadae mfalme alizungumza na Bwana Vuai juu ya shida iliyompata kutokana na mtoto wake, hivyo ninakiri umasikini wako na kwamba nitakujengea nyumba yako na nitakusaidia kama ipasavyo lakini mtoto wako amuoe mtoto wangu, kwa sababu ninaridhika vya kutosha. Na hapo Bwana Vuai alikubaliana na mfalme na wakaandikiana mkataba kuhusu hayo waliyoyazungumza.

Ilipofi ka siku ya sita mfalme alifi ka na zana zote, na kuanza shughuli za ujenzi. Na baada ya siku kidogo nyumba ilimalizika na kwenda kufunga ndoa. Hapo tena baada ya ndoa mtoto wa mfalme alipoa matatizo yake na hatimae mtoto wa Bwana Vuai alipewa mali nyingi sana na mfalme na unyonge pamoja na umasikini waliokuwa nao awali ukaondoka na akawa wakati wowote anaruhusiwa kwenda kuwaona wakwe zake.

HADITHI!! HADITHII!!!

WIZI MBAYA

Imesimuliwa na Zubeda Abdalla Omar.
Hapo zamani za kale alikuwepo bwana mmoja, aliekuwa na wake watatu mmoja alikuwa mwizi. Yule
bwana alikuwa anafuga mbuzi, siku moja kati ya wale wake zake mmoja aliiba mbuzi na kumchinja na kumpika bila ya yeye kujua. Aliporudi safari yake aliuliza nani alimchinja mbuzi? Wote walikataa. Yule bwana akasema basi mimi nitafanya dawa. Wakajibu sawa, yule bwana akafanya mambo yake kisha akawapeleka mtoni. Walipofika aliwambia  mmoja mmoja aanze  kuingia mtoni na huku akiimba.
Aliingia wa kwanza huku akiimba nyimbo:
     Kachiriri, kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri. 
     Mani nenga Kachiri
     Depala dipolo kachiri
     Dipolo dabambo kachiriri
     Kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri.
Alipomaliza kuimba akaibuka, kwani yeye hakuwa mwizi. Akafuata wa pili huku akiimba:
     Kachiriri, kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri. 
     Mani nenga Kachiri
     Depala dipolo kachiri
     Dipolo dabambo kachiriri
     Kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri.
Yeye pia akaibuka na kukaa pembeni.  Akafuata yule wa tatu akaingia huku akiimba:
     Kachiriri, kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri. 
     Mani nenga Kachiri
     Depala dipolo kachiri
     Dipolo dabambo kachiriri
     Kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri.
Lakini yeye alizama.
Kuona vile yule bwana akajua kwamba yule mke wa tatu ndie mwizi. Hapo akafanya dawa zake na yule bibi  akaibuka, alimuomba radhi mumewe na kuahidi kuwa  hatorudia tena kosa lake. Na yule bwana alikubali na wakaendelea kuishi kwa raha mustarehe.


DAMU NZITO KULIKO MAJI

Damu ni nzito kuliko maji

                




Methali: Damu ni nzito kuliko maji damu blood      maji - water Meaning: Blood is thicker than water.
Application: It is important to keep family ties last forever.
 

Friday, 28 October 2016

THE TOP TEN SCHOOLS AND STUDENTS IN STANDARD SEVEN RESULTS 2016

Ufaulu kwa watahiniwa wa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi 2016 umepanda kwa asilimia 2.52 kutoka asilimia 67.84 mwaka jana hadi asilimia 70.36, huku wavulana waking’ara katika matokeo hayo ambao wengi wametoka shule za Kanda ya Ziwa.
Matokeo hayo yaliyotangazwa jana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk Charles Msonde ambaye alisema kati ya wanafunzi 10 bora waliofanya vizuri katika mtihani huo, msichana ni mmoja tu, Justina Gerald wa Shule ya Msingi ya Tusiime ya jijini Dar es Salaam.
Kati ya wanafunzi hao 10, watahiniwa saba wanatoka Shule ya Msingi Kwema iliyopo mkoani Shinyanga, wawili Tusiime na mmoja kutoka Kaizirege ya Bukoba mkoani Kagera. 
Dk Msonde alisema jumla ya watahiniwa 555,291 kati ya 789,479 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa kupata jumla ya alama 100 na zaidi kati ya alama 250.
“Idadi hii ya watahiniwa waliofaulu ni sawa na asilimia 70.36, kati ya hao wasichana ni 283,751 na wavulana 271,540. Mwaka 2015 ufaulu ulikuwa ni asilimia 67.84 kuwapo ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2.52,” alisema Dk Msonde.
Watahiniwa 16,929 wamepata daraja A, watahiniwa 141,616 wamepata Daraja B, watahiniwa 396,746 wamepata daraja C, watahiniwa 212,072 wakipata daraja D na 21,872 wakipata daraja E . 
Dk Msonde alisema ufaulu katika masomo ya Sayansi na Maarifa ya Jamii umepanda kwa asilimia kati ya 4.06 na 14.76 ikilinganishwa na mwaka 2015 huku masomo ya Kiswahili, Hisabati na Kiingereza ufaulu umeshuka kwa asilimia kati ya 0.39 na 12.51 ukilinganisha na mwaka jana.
“Watahiniwa wamefaulu zaidi katika somo la Kiswahili ambalo ufaulu wake ni asilimia 76.81 na somo walilofaulu kwa kiwango cha chini ni Kiingereza lenye ufaulu wa asilimia 36.05,” alifafanua Dk Msonde.
Dk Msonde aliwataja watahiniwa waliofanya vizuri na shule zao kwenye mabano kuwa ni:
  • Japhet Stephano, Jamal Athuman na Enock Bundala (Kwema),
  • Justina na Shabani Mavunde (Tusiime),
  • Jacob Wagine, Isaac Isaac, Daniel Kitundu na Benjamin Benevenuto (Kwema)
  •  Azad Ayatullah (Kaizirege).
Wasichana 10 bora:
  1. Justina Gerald (Tusiime)
  2.  Danielle Onditi (Tusiime)
  3. Linda Mtapima (Kaizirege),
  4. Cecilia Kenene (Mugini),
  5. Magdalena Deogratias (Rocken Hill),
  6. Asnath Lemanya (Tusiime),
  7. Fatuma Singili (Rocken Hill),
  8. Ashura Makoba (Kaizirege),
  9. Rachel Ntitu (Fountain of Joy),
  10. Irene Mwijage (Atlas)
Wanafunzi wavulana 10 bora kitaifa,
  1. Japhet Stephano (Kwema),
  2. Jamal Athuman (Kwema),
  3.  Enock Bundala (Kwema),
  4. Shabani Mavunde (Tusiime),
  5. Jacob Wagine (Kwema),
  6. Isaac Isaac (Kwema),
  7. Daniel Kitundu (Kwema),
  8. Benjamin Benevenuto (Kwema),
  9. Azad Ayatullah (Kaizirege)
  10. Benezeth Hango (Kwema).
Shule 10 bora ni:-
  1. Kwema (Shinyanga),
  2. Rocken Hill (Shinyanga),
  3. Mugini (Mwanza),
  4. Fountain of Joy (Dar es Salaam),
  5.  Tusiime (Dar es Salaam),
  6. Mudio Islamic (Kilimanjaro),
  7. Atlas (Dar),
  8. St Achileus (Kagera),
  9. Giftskillfull (Dar),
  10. Carmel (Morogoro).
Shule 10 ambazo hazikufanya vizuri ni:-
  1. Mgata (Morogoro)
  2. Kitengu (Morogoro)
  3. Lumba Chini (Morogoro),
  4. Zege  (Tanga),
  5.  Kikole (Tanga),
  6. Magunga ya Morogoro,
  7. Nchinila (Manyara),
  8. Mwabalebi (Simiyu)
  9. Ilorienito (Arusha)
  10. Chohero (Morogoro)
Mikoa 10 iliyoongoza kitaifa ni Geita, Katavi, Iringa, Dar es Salaam, Kagera, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha, Njombe na Tabora wakati Halmashauri 10 bora ni Mpanda Manispaa, Geita Mji, Arusha Mji, Mafinga Mji, Chato, Mwanza Jiji, Moshi Mji, Mji Makambako, Ilemela na Hai.

WAHENGA WETU!!

Ganda la muwa la jana, chungu kaona kivuno 
Ganda la jana la muwa huwa limekauka, lakini chungu anapolipata huona ni mavuno maridhawa. Maana asiyezoea kuwa nacho, akipatapo hata kama ni kitu duni au hafifu namna gani na kidogo, hushangilia. Mathalani, kukengeuka kwa maadili kwa vijana barani Afrika na kuzamia tamaduni za kigeni.

Milima haikutani, lakini binadamu hukutana
Milima haina uwezo wa kukutana, lakini binadamu wakiwa hai huweza kukutana hata baada ya kuwa mbalimbali kwa muda mrefu. Hii ni methali inayotumika katika kutiana moyo wakati wanapoagana kwamba wakijaliwa watakutana. Pia hutumika katika kuwaonya watu kuacha tabia ya kuwatendea vibaya wengine kwani huenda wao pia wakatendewa hivyo siku za usoni. 

SHULE YA KWANZA KITAIFA

TAZAMA MATOKEO YA SHULE YA KWANZA KITAIFA MWAKA 2016 KATIKA MATOKEO YA DARASA LA SABA


Thursday, 27 October 2016